Jumapili, 31 Agosti 2014

VILE MUNGU ANAVYO KUJUA NI ZAIDI YA MWANADAMU ANAVYO KUJUA

VILE MUNGU ANAVYO KUJUA NI ZAIDI YA MWANADAMU ANAVYO KUJUA:
NI ZAIDI YA HATA SISI TUNAVYO JIJUA:
NI ZAIDI YA WEWE UNAVYO JIJUA MWENYEWE:



Kibari chako kiko katika mema unayo yafanya siku zote
haswa  katika kazi ya MUNGU
MUNGU anafahamu makusudio ya mwanadamu kabla ajafika katika jambo ambalo wenda angelifanya wiki,mwezi,au hata mwaka unaokuja
MUNGU aliona kusudio la kaini alipo taka kumuangamiza nduguye Habili,akamwambia  kuna dhambi ina kutamani hapo baadae
MWA4:6-8
BWANA akamwambia kaini ,kwanini una ghadhabu? na kwanini uso wako umekunjamana?kama ukitenda vyema utapata kibari?Usipo tenda vyema dhambi iko,inakuotea mlangoni,nayo inakutamani wewe,walakini yapasa uishinde.
Ni kwamba MUNGU aliona kilicho kuwa mbele ya kaini akamwambia inapasa uishinde,tabu juu yetu hatuifahamu sauti ya MUNGU,na kama tunaifahamu tunafanya ugumu wa mioyo

Nitakuambia MUNGU anapateje kujua na kuona sili zako ambazo hata wewe haujui nini kitatokea hapo baadae
Alikuwepo nabii mmoja ,baada ya MUNGU kuiona safari yake kuwa si salama alimwambia usile,usinywe,wala usirudie njia uliyo itokea maana MUNGU aliona, nini kitakacho mpata iwapo ata kwenda kinyume na maagizo hayo, yeye mwenyewe hakufahamu lo lote hata alipodanganywa alikubali.
1FALM 13:16-17
Nae akamwambia,siwezi kurudi pamoja na wewe,wal kuingia pamoja na wewe;wala sili chakula,wala sinywi maji pamoja nawe hapa, kwani nimeambiwa,kwa neno la BWANA,
Usile chakula ,wala usinywe maji huko,wala usirudie kwa njia ile ulioijia

MUNGU alifahamu Mtu huyu asipoenda hivyi atapatwa na madhara makubwa aidha mauti
Msikilize MUNGU ndiye aliye na njia zako bila MUNGU hakuna kitu ni kama gari bila dereva gizani
Hata YESU alipo waagiza petro na yohana,kuandaa pasaka walishindwa ,wtaandaa wapi,ikabidi waulize  ndipo akawaambia
LK 22:9-10
Wakamwambia wataka tuandae wapi?Akawaambia tazama, mtakapoingia mjini mtakutana na mwanamume akichukuwa mtungi wa maji, mfuateni mkaingie katikanyumba atakayoingia yeye
walikuwa hawafahamu lolote ,lakini kwa yesu picha na umbo la hiyo pasaka lilikuwa moyoni,si kwamba labda aliwahi kwenda na kufanya mawasiliano au kumuomba yule mwenye mtungi, hapana yeye kwa uwezo wake alifahamu
mifano hii najaribu kukuonyesha kuwa MUNGU anaona na kufahamu kabla yako wewe hujafahamo lolote
Pia kama vile MUNGU alivyo fahamu mawazo ya Kaini vivyo hivyo alifahamu mawazo ya Yusufu juu ya mke wake Mariamu alipo kusudia kumuacha,pia mwana mke msamari aliyekutana naye kisimani
YN 4:15
Yule mwanamke akamwambia BWANA unipe hayo maji nisione kiu wala nisije hapa kuteka, YESU akamwambia nenda kamwite mumeo uje naye hapa.Yule mwanamke akajibu akasema sina mume
{YESU akamwambia umesem vyema sina mume .Kwamaana umekuwa na waume watano naye uliye naye sasa siye mume wako,hapo umesema kweli}
MUNGU anafahamu kusudi lako,PETRO alijiona kwakuwa yuko na yesu na watu walivyo msifia kuwa ,unafanana na YESU alijenga kiburi na kuona kila jambo anaweza YESU akamwambia PETRO wewe utanikana maratatu kabla jogoo ajawika,maana aliangalia kwa uzoefu wake akaona imani ya PETRO bado,kwahiyo tunapo patwa na hali ngumu huwa tuna mkana YESUna YESU anajua kabisa kuwa utamkana
nimalize mpendwa wangu kwa kukupa sababu za MUNGU anapateje kujua mambo juu yako unayo yawaza na yatakayo kutokea baadae au siku za usoni,kamavile MUNGU alivyo ona hatari iliyo taka kumpta mkulima,aliyesema Ee nafsi yangu tulia sasa ule na kunywa MUNGU akamtokea akamwambia, mpumbavu wewe leo wanitaka roho yako,Hicho ulichojiwekea hakiba kitakuwa cha nani?niache huko maana si lengo tika lengo;
MIT 20:27
Pumzi ya mwanadamu ni taa ya BWANA; Hupeleka yote yaliyo ndani yake
Kwahiyo mpendwa wangu ,yote yote utakayo waza ujawaza umeona ujaona taalifa yake inaenda,tena unaipeleka mwenyewe,je ni nini utakacho kifanya asijue MUNGU? au katika mabaya utajificha wapi usionekane na bwana?kwakuwa MUNGU wetu ana tupenda ,anapoona jambo la hatali katika taalifa yako,anakuhimiza omba kama umeokoka na mana ujaokoka anakuhimiza okoka,
yeye husema na kila mmoja awe ameokoka au ajaokoka.labda pumnzi yako ikome au usiitumie pumzi ya mungu,kama itawezekana,na ninajua ni ndoto,kwahiyo ili uishi salama wewe ambaye umeokoka ni kujaza maneno ya MUNGU moyoni ili ikienda taalifa iendea yenye utukufu
Nawewe ambaye bado ujaokoka sikutishi bali ninakuomba uchukuwe hatua ya karibu na umpokee YESU ili ukurasa wako ubadilishwe na inapokwenda taalifa iwe ni utukufu
usijidanganye,hatakama ujaokoka taalifa inaenda aiajalishi uko katika hali gani
MUNGU AKUBARIKI SANA NA UZIDI KUSONGA MBELE


Mwinjilisti JOHANNES R MNIKO
0712  565 676                                   Askofu doct BARNABAS I KIMBE
    PGMM                                                       0653 395 344/0754 395 344
VINGUNGUTI                                                    PGMM
DSM                                                                  VINGUNGUTI 
                                    KARIBUNI
Najua wengi mnamzigo wa kuwaeleza watu wa MUNGU maneno ya uponyaji basi tuwasiliane ili utumie blogg hii kwa kukiokoa kizazi hiki ambacho shetani anajisifu kuwa amekimiliki,tumika ili watu wa MUNGU wapone,pia kama tuko pamoja LIKE 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni