Jumanne, 29 Julai 2014

NEEMA YA MUNGU NA HURUMA ZAKE KWETU

TANGU ADAMU WA KWANZA HATA ADAMU WA SASA :
WAMEJENGWA NA KUTO JARI;HATA KUYAPUUZA MAAGIZO,AMRI NA MASHAULI:



           Nikweli kuwa kibuli na dhalau pamoja na kutojali kunafanya binadamu kujengeka na kiburi
mfano: kutojari mtuanapoambiwa jambo anasema nita tenda,afu anakamatwa na uvivu furani na                        anajikuta hajatenda
           sio yeye ni vile amekubari afu hajachukuwa hatua, na shetani hutumia nafasi hiyohiyo                          kuwakosanisha
             
mfano: MUNGU alipomwambia ADAMU mitiyoote matunda yake waweza kula lakini huu tuu usile                    hakika siku utakayo kula utakufa,
           shetani alipo isikia ile HAKIKA akaifanyia kazi
MUNGU anaposema jambo huwa amelidhibitisha ni kweli halitokengeuka wala kubadilika
 Angalia HAKIKA aliyosimamia:
MWA 3:5
       Kwamaana MUNGU anajua ya kwamba siku ile mtakayo kula matunda ya mti huo,mtafungliwa macho,nanyi mtakuwa kama MUNGU,mkijua mema na mabaya.
hii ndiyo HAKIKA aliyosimamia shetani


EBU jiulize shetani baada ya kutenda dhambi pamoja na ADAMU wa kale, hadi leo anatumikia hadhbu aliyo adhibiwa, anakwenda kwa tumbo,anakula mavumbi pia
Lakini mwanadamu anataka kulahisisha hadhabu ya MUNGU

mfano
         mwanaume aliambiwa atakula kwa jasho lakini kwa mwanaume inakuwa ni ngumu
yeye anataka apate vya lahisi lahisi visivyo mtoa jasho sawa, anafanikiwa lakini baraka za MUNGU hazipo hapo wala mkono wa MUNGU haupo hapo mwanzo 3:17

mwanamke yeye aliambiwa utazaa kwa uchungu,lakini leo wanamama wengi wanapo taka kujifungua anaenda kwa waganga ili ajifungue salaama wengine hudiliki kwenda kwao katika mizimu kuiomba imsaidie aliisha sahau kuwa kuzaa kwa uchungu ni agizo la MUNGU

Jambo lingine ni vyakula hapo sasa ndipo tumekengeuka kabisa
MWA 3:17
               Akamwambia adamu,kwakuwa umeisikiliza sauti ya mke wako,ukala matunda ya mti ambao nilikuagiza,nikisema Usile:ardhi imelaaniwa kwa ajili yako:kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako ;michongoma na miiba itakuzalia,nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula,hata utakapo irudia ardhi,ambayo katika hiyo ulitwaliwa;kwa maana u mavumbi wewe,,nawemavumbini utakwenda

hili ni agizo kijana wa leo wao ni kijiweni halijui agizo, lakini pamoja na agizo hili mwanadamo wa leo kaachia nafasi na shetani akaitumia nafasi hiyo pamoja na mawazo yetu na tunakuta tuna fanya jambo sikuzote halimpi MUNGU utukufu

jambo lingine ni mitandao ya kijamii ivi kweli kama kweli kwa haya yanayo fanyika leo MUNGU je ana tufikiliaje? je? hilo ndilo agizo,tusidanganyike na neema iliyoko mbele yetu

hakuna kujificha kwa matendo yako,kuna wengi wanasema nimeokoka nampenda YESU lakini haendani na maneno hayo ,nataka nikuambie rafiki yangu utamficha mwanadamu lakini kwa MINGU uko uchi afadhari na ulipo zaliwa ulisitiliwa,kwa MUNGU uko uchi
 MITHARI 20:27
                    Pumzi ya mwanadamu ni  taa ya BWANA,
                     Hupeleka yote yaliyomo ndani yake
Lolote unalo waza ndg yangu,taarifa inaenda
liwa jema au baya hakuna siri kwa MUNGU  
MUNGU wangu wa mbinguni na akubariki sana 

Mwinjilist  Johannes R Mnico
0712565676
PGMM church
VINGUNGUTI 
D,Salaam 
                                                           Askof, BARNABAS I KIMBE
                                                                     0754395344/0653395344
                                                                      PGMM Chur chu 
                                                       PENTEKOST GOSPEL MISSION &MINISTERS

Ijumaa, 25 Julai 2014

MBASHA NA FLORA WAPATANA NA KUISHI PAMOJA TENA


MBASHA, FLORA WAPATANA


Ule mtafaruku ndani ya ndoa ya mwimba Injili mahiri Bongo, Flora na mumewe, Emmanuel Mbasha umedaiwa kumalizika kwa wawili hao kupatana, Risasi Jumamosi linakuwa nambari wani kukuhabarisha.
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, wawili hao walikalishwa kikao cha upatanishi mapema wiki hii kilichokuwa chini ya familia.
Mume wa Flora Mbasha, Bw. Emmanuel Mbasha.
MANENO YA CHANZO
“Kikao cha familia kilikaa, Mbasha aliitwa akafika, Flora naye aliitwa akatokea, mazungumzo yalikuwa marefu lakini kimsingi waliamua kuweka kando mtafaruku wao na kuijenga upya ndoa yao,” kilisema chanzo.
Chanzo kiliongeza kuwa katika kikao hicho cha mwanzoni mwa wiki hii, miongoni mwa adidu za rejea ilikuwa kutokumbushia vikao vilivyopita ambapo hakukupatikana muafaka.
VIKAO VILIVYOPITA
Katika vikao vilivyopita, wahusika wakuu walikuwa wazazi wa Mbasha (mzee Maneno Mbasha, Zulfa Maneno), ndugu wa Flora na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
Mwimbaji Injili mahiri Bongo, Flora Mbasha.
VIKAO VYA BAADAYE
Kwa mujibu wa chanzo, vikao vilivyofuata, wawili hao wakawa tayari kila mmoja ametema nyongo yake pembeni na kufikia makubaliano kwamba, ndoa yao isimame tena wakitumia maandiko kwenye Biblia kutoka kitabu cha Waebrania yanayosema:    Ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.
WAKORINTHO YAFUNGA KAZI
Kwa mujibu wa chanzo hicho, maneno mengine ya Biblia yaliyotumika kwenye kikao hicho mpaka wawili hao wakaamua kurudiana ni 1 Wakorintho 7:1-10 ambapo maandiko yanasema:
Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe. Mume na ampe mkewe haki yake vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.
Flora Mbasha akiwa kwenye picha ya pamoja na mumewe, Emmanuel Mbasha.
Mke hana amri juu ya mwili wake bali mumewe vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake bali mkewe. Msinyimane, isipokuwa mmepatana kwa muda ili mpate faragha kwa kusali, mkajiane tena shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.
Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza, wala hapo si mimi, ila Bwana (Mungu), mke asiachane na mumewe, lakini ikiwa ameachana naye na akae asiolewe au apatane na mumewe, tena mume asimwache mkewe.
KIKAO CHA JUMAMOSI KUMALIZIA
Chanzo kilisema kuwa, kikao cha mwisho ambacho kitamalizia kuweka mambo sawa ili wawili hao waanze ngwe ya pili ya ndoa yao ambayo inaaminika itakuwa ya mwisho mpaka kifo kiwatenganishe, kinatarajiwa kufanyika leo jijini Dar es Salaam mahali ambapo hapakutajwa.
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
MWANASHERIA ATAJWA
Mwanasheria wa Flora aliyejulikana kwa jina moja la Ado ametajwa kusimamia kikao hicho ili wawili hao waanze maisha mapya baada ya safari fupi ya mvurugano uliowafanya kuwa mbalimbali.
AONGEA NA RISASI JUMAMOSI
Juzi, Risasi Jumamosi lilimsaka mwanasheria huyo kwa njia ya simu yake ya mkononi ili kumsikia anasemaje kuhusu kutajwa kwenye usuluhishi wa ndoa hiyo ambapo alipopatikana alisema:
“Niko Arusha, Ijumaa nitarudi Dar. Kuhusu kikao cha usuluhishi siwezi kukwambia lakini suala la kuwapatanisha nalifahamu, nawaomba na ninyi msaidie kufanikisha jambo hilo zuri.”
VIPI KUHUSU KESI YA MADAI YA KUBAKA?
Hata hivyo, Wakili Ado hakutaka kugusia kuhusu kesi ya Mbasha iliyopo Mahakama ya Wilaya ya Ilala ambapo anadaiwa kumbaka shemejiye mara mbili (jina tunalo) ambayo kwa mujibu wa mahakama, upelelezi umekamilika na itasikilizwa Julai 17, mwaka huu.
KWA UPANDE WAKE FLORA
Risasi Jumamosi lilimwendea hewani, Flora ili kumsikia anasemaje kuhusu kuwepo kwa upatanishi kati yake na mumewe, Emmanuel.
Huyu hapa: “Ongea na wakili wangu atakwambia kila kitu.” Ambapo majibu ya wakili yalikuwa: ”Ninachojua mimi ni kwamba Flora ameshamsamehe mumewe na yuko tayari kuanza ukurasa mpya.”
MBASHA SASA
Kwa upande wake, Mbasha alipozungumza na gazeti hili juzi alisema kurejea upya kwa ndoa yake ni jambo la kuupendeza moyo wake.
“Mimi sina neno nipo tayari, nimeshasamehe yaliyotokea, Flora ni mke wangu jamani, nampenda sana kutoka moyoni.” 

Alhamisi, 24 Julai 2014

IMANI NI SEHEMU AMBAYO WAKRISTO TUMEIPOTEZA:

WAKRISTO TUMEPOTEZA SEHEMU MUHIMU SANA
AMBAYO HATUWEZI KUFIKIA VITU VYA ROHONI PASIPO HIYO IMANI: 

Watanzania wenzangu, ususani wakristo kuna jambo ambalo linalo achiliwa furaha na MUNGU wetu kuja kwetu kama unaishi na IMANI na sio kuwa na IMANI maana YESU alisema ,ukiwa na IMANI kama punje ya haradani unaweza kuuambia mlima huu ng'oka nao ukatii VITUVYOTE BILA IMANI HAIWEZEKANI unapokuwa na imani unampendeza MUNGU kuna vitu ambavyo MUNGU ameahidi ambavyo tunavipokea kwa imani

ukisoma kumbu kumbu la torati 28 kunavitu vingi ambavyo utekelezaji wake ni IMANI je? unajuwa ni kwanini IBRAHIMU aliupendeza moyo wa MUNGU ? ni kwa sababu alikuwa na imani na alimwamini saana MUNGU na ndo maana alipata hata nafasi ya kuitwa rafiki wa MUNGU

LUKA mwanafunzi wa YESU, baada ya kuijua imani alidiliki kuandika yale ambayo YESU alisema mwenyewe
LK 21:15
              Kwasababu mimi nitawapa kinywa na hekima ,ambayo watesi wenu wote  hawata weza kushindana nayo wala kuipinga 

lakini sasa huwezi kupokea siraha hii kubwa pasipo kuwa na IMANI maana hivi vyote umekwisha kupewa lakini hatuja pokea  kwa kuwa hatuna IMANI
Mwenye IMANI  anafundishika,hata MUNGU uingilia kati juu ya mafundisho yake,mpenda ni MUNGU anaye achilia vyote kukufuata ;afuataye baraka hana imani, aliye na imani atavumilia kila hali,akimtumai MUNGU
YESU alisema na wote watakuwa wamefundishwa na MUNGU Ili kuishikilia IMANI yao
YN 6:45 
             Imeandikwa katika manabii, na wote watakuwa wamefundishwa na MUNGU,basi kila aliyesikia na kujifuza kwa BABA Huja kwangu,

kwahiyo imani inajengeka kabla ya kumjua YESU na unapo  okoka ndipo unazidi kukua ki IMANI,
Lakini pia leo tunaye ROHO mtakatifu ndiye anayefanya kazi ya kutupandikizia IMANI
IMANI inazaa vitu vingi sana,

mfano :hekima,maalifa,uaminifu,upendo, utu wema,kujari,na vingine vingi
YAKOBO asema ukipungukiwaq na hekima uombe dua lakini dua yenyewe ni lazima uwe na IMANI Maana maandiko yanasema kila amwendeaye MUNGU ni lazima aamini yupo kwahiyo lazima uamini

YAKO 1:5  
                 Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa MUNGU awapae wote kwa ukalimu, wala hakemei;naye atapewa 
Utapewa kama utakuwa na imani na kuamini juu ya lile uombalo,usijaribu, IMANI haijaribiwi
BWANA YESU asifiweeeeeeeeeee,,! Haleluyaaaaaaaaaa,,!
amina na MUNGU akuhifadhi na kukutetea  mpendwa wangu
tuombe,,,! 
                             BABA katika jina la YESU KRIST O 
                              ninamuweka msomaji wa nakala hii 
                              mikononi mwako ukamjaze imani 
                              ya kweli na tumaini la mbinguni  
                               ukamkumbuke pia katika uzima 
                                  wa milele na haja ya moyo wake ukampe 
                            ni katika jina la YESU  KRISTO 
                                    nimeomba na kuamini 
                                          Imeen...!
mwinjilisti Johannes R mnico
0712565676 
PGM CHURCH 
VINGINGITI 
                                Askofu, BARNABAS, I ,KIMBE
                                 0754395344 / 0653395344
                             KARIBU  PENTEKOST GOSPEL MISSION
                                  Huduma zote za ki ROHO zinapatikana

nyimbo

Kibwagizo (Chorus)
Milele, Milele, Milele eeee,
Milele, Milele, Milele eeee,
Milele eeee, Milele, Milele eeeee,
Milele eeee, Milele, Milele eeeee,
Aaah,
Aaaah, Nitalisifu Jina Lako Bwana,
Aaaah, Nitalisifu Jina Lako oooh,
Aaaah, Nitalisifu Jina Lako Bwana,
Aaaah, Nitalisifu Jina Lako oooh,
Beti 1
Hakika Upendo wako, ooooh
Nashindwa kuupima mimi,
Ulinipenda mimi, iiiih,
Ukatoa uhai wako,
Yote hii Bwana, aaaah
Uniepushe na mateso,
Yote hii Bwana, aaaah
Uniepushe na kuzimu,
Ukaja duniani, iiiih,
Ukapata mateso mengi,
Ulijishusha sana, aaaah,
Ili utukomboe sisi,
Mimi sijaona, aaaah
Upendo kama wako tena
Mimi sijaona, aaaah
Upendo kama wako tena
Nasema, Milele, Milele Nitalisifu Jina Lako
Kibwagizo
Milele, Milele, Milele eeeee,
Milele, Milele, Milele eeeee,
Milele eeee, Milele, Milele eeeee,
Milele eeee, Milele, Milele eeeee,
Aaah,
Aaaah, Nitalisifu Jina Lako Bwana,
Aaaah, Nitalisifu Jina Lako oooh,
Aaaah, Nitalisifu Jina Lako Bwana,
Aaaah, Nitalisifu Jina Lako oooh,
Beti 2
Niwapo mashakani, iiiih
Rafiki hunikimbia,
Niwapo ni mgonjwa, aaaah
Watu husema pole sana,
Lakini hawawezi, iiiih
Kutatua shida zangu,
Lakini hawawezi, iiiih
Kutatua shida zangu,
Peke yako nakuona, aaaah
Waja kunifariji moyo,
Peke yako nakuona, aaaah
Waja kutibu afya yangu,
Peke yako nakuona, aaaah
Wanitendea miujiza,
Ndio maana nasema, aaaah
Una upendo mwingi sana,
Ndio maana nasema, aaaah
Una upendo mwingi sana,
Kibwagizo
Milele, Milele, Milele eeeee,
Milele, Milele, Milele eeeee,
Milele eeee, Milele, Milele eeeee,
Milele eeee, Milele, Milele eeeee,
Aaah,
Aaaah, Nitalisifu Jina Lako Bwana,
Aaaah, Nitalisifu Jina Lako oooh,
Aaaah, Nitalisifu Jina Lako Bwana,
Aaaah, Nitalisifu Jina Lako oooh,
Beti 3
Wale walio yatima,
Umekuwa baba yao,
Wale walio wajane,
Umekuwa mume kwao,
Wewe wawashindia, aaaah
Katika magumu yote,
Haijarishi wanadamu, uuuuh
Wamewatenga mbali sana,
Unawakumbatia, aaaah,
Wawapa mahitaji yao
Unawakumbatia, aaaah,
Wawapa mahitaji yao
Nasema, Milele, Milele Nitalisifu Jina Lako
Kibwagizo
Milele, Milele, Milele eeeee,
Milele, Milele, Milele eeeee,
Milele eeee, Milele, Milele eeeee,
Milele eeee, Milele, Milele eeeee,
Aaah,
Aaaah, Nitalisifu Jina Lako Bwana,
Aaaah, Nitalisifu Jina Lako oooh,
Aaaah, Nitalisifu Jina Lako Bwana,
Aaaah, Nitalisifu Jina Lako oooh,

KAATIKA UUMBAJI RUSFA ALIHUSIKA:


Wakati wa uumbaji, Lusifa alihusika vipi?


…natuumbe Mtu kwa mfano wetu…..” hiyo haimaanishi kwamba alikuwa akijiambia katika kikao chake Mungu mwenye nafsi tatu zilizo sawa! Kimsingi, Mungu alipokuwa akisema juu ya kumuumba Mtu, alikwisha muumba tayari katika mawazo yake, kabla ya kusema tamko lake hilo. Siku hiyo alipotamka juu ya mpango wake wa kumuumba Mtu ilikuwa ni kuweka wazi mpango wake huo na pia kuonyesha makusudi yake katika uumbaji huo.

Lakini kiukweli mkutano huo ulikuwa baina ya Mungu na Lusifa wakiwepo na malaika wote wa mbinguni, na mkutano huo ulimlenga Lusifa! Labda kabla sijaendelea niseme ni kwa nini; Kwa mjibu wa ile Mw.1:26. Hebu jiulize, kama Mungu ni nafsi tatu, na kwamba utatu huo ndiyo Mungu mmoja; je, inawezekanaje Mtu mmoja tena anayejua yote, anayeweza na Mfanya yote afanye mkutano, na kujiambia peke yake juu ya mpango Fulani aliokwisha ubuni peke yake na anatazamia kuufanya peke yake? ukiendelea ule mstari wa 27, utaona upekee wa Mungu!

Ukiendelea katika kuipeleleza Biblia utaona kuwa; Kimsingi, Mungu katika uumbaji wa huyo Mtu wa kwanza, alipenda kumshirikisha pia Lusifa kwa kuuweka wazi mpango wake huo ili kuuibua ule uovu uliokuwemo katika moyo wa Lusifa mbele ya malaika watakatfu wa mbinguni. Na kama yangetokea mapatano kati yake na Lusfa, kule kuwapo tu makubaliano japo utendaji unabakia kuwa wa Mungu, basi na Lusifa angeshiriki kumuumba Mtu! Kama hutajari ukiiangalia vema na kwa utulivu Biblia yako, bila kutanguliza ujuzi wako mwenyewe, utuona mpango mzima wa umbaji wa Mungu hadi katika lile shamba, ambalo Yule Mtu alikwenda kuishi ambako pia na huyo Lusifa alikuweko, utaona kuwa Sababu kubwa ya Mungu kuitisha kikao hicho cha “uumbaji Mtu” ulilenga kuweka wazi tofauti ambazo Mungu alikwisha ziona moyoni mwa Lusifa, naaliyekuwa akiambiwa “…natuumbe mtu kwa mfano wetu alikuwa huyohuyo Lusifa, Biblia inasema, Lusifa hakukubaliana na mpango huo na hivyo akakataa na kuwa mwasi.

Tangia hapo nafasi na kiti chake akanyang’anywa na kutupwa hapa Duniani. Naye akawa mmoja wa watawala katika hii Dunia sawa sawa na TAMAA yake! Lakini, kama ilivyo katika mabalaza na serikali za wanadamu, kiongozi anaweza kuamua kufanya jambo, na kuwashirikisha washirika wake na kuita jambo hilo wanalifanya wote! Pengine utasema ilikuwaje akasema “…Natuumbe mtu kwa mfano wetu” je, malaika nao ni mfano wa Mungu kwa vipi? Ndiyo, nao ni mfano wa Mungu! Ndiyo maana Mungu akasema “kwa mfano wetu” je, mfano wa Mungu ni upi au mfano huo ni nini aliotufanya nao ambao na Malaika pia wanao? Jibu tunalipata katika Efe.4:23-24, inasomeka hivi “Na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli” Mfano wa mungu tuliyoumbwa nao na ambao na malaika, na hata Lusfa ambaye sasa ni Ibilisi na shetani alikuwa nao ni HAKI NA UTAKATIFU WA KWELI! Kwasababu ya mda ningekuolodheshea maandiko mengi tu yanayokubali kuwa Mungu ni MMOJA tu!

Jumatano, 23 Julai 2014

Jesus is NOT Coming BACK – Roman Catholic Leaders SAID

  • 32K
     
    Share
vaticanA SPOKESPERSON for the Vatican (Roman Catholic) has officially announced today that the second coming of Jesus, the only son of the God, may not happen now after all, but urged followers to still continue with their faith, regardless of the news.
Cardinal Giorgio Salvadore told WWN that this years 1,981st anniversary is to be the Vatican’s last in regards to waiting for the Lord to return to Earth.
“We just feel Jesus is not coming back by the looks of it.” he said. “It’s been ages like. He’s probably flat out doing other really good things for people somewhere else.”
Nearly two thousand years ago, Jesus promised his disciples that he would come again in chapter John 14:1-3 of the bible: “There are many homes up where my Father lives, and I am going to prepare them for your coming. When everything is ready, then I will come and get you, so that you can always be with Me where I am. If this weren’t so, I would tell you plainly”
The Vatican defended Jesus’ broken promise, claiming “he was probably drinking wine” at the time when he made the comments.
“Having the ability to turn water into wine had its ups and its downs.” added Cardinal Salvadore. “We all make promises we can’t keep when we’re drunk. Jesus was no different.”
The church said it will now focus attentions on rebuilding its reputation around the world, but will keep an optimistic mind for the savior’s second coming.
mzansidaily.co.za
- See more at: http://www.eacvision.com/news/jesus-is-not-coming-back-roman-catholic-leaders-said/#sthash.PsUBsqPC.dpuf

Jumanne, 22 Julai 2014



Yule Mshindi wa Tuzo za Groove Awards kwa upande wa Wanaume, Na pia Mshindi katika Easter Africa Gospel Music Awards, na Pia Mshindi katika Africa Gospel Music Awards Daddy Owen amejitoa katika Kinyang'anyiro cha Groove Awards 2012 ili kuweza kupisha Chipukizi kuweza kuchukua Tuzo hizo Mwaka 2012.

Pamoja na Daddy Owen Kujitoa Jina lake limeendelea kupigiwa kura na mashabiki wake wakimtaka Mkali Huyo wa Gospel Africa Mashariki Kurudi Ulingoni kutoa Changamoto.Daddy Owen anayetamba na Kibao Chake Cha "Dakika Tatu" amekuwa gumzo katika mashindano hayo mwaka huu.

Mwaka Jana katika Mashindano hayo kwa wanamuziki Kutoka Tanzania mshindi aliibuka Christina Shusho na kutwa taji hilo, mwaka huu katika Category ya Wanamuziki Kutoka Tanzania yuko Rose Muhando, Bon Mwaitege, Bahati Bukuku, Christina Shusho na Neema Mushi. Mpaka sasa Mchuano Mkali katika Kura upo kwa Rose Muhando pamoja na Christina Shusho katika Kundi la Tanzania.


MALE ARTIST OF THE YEAR
Man Ingwe Mshiriki mmojawapo katika Category Male Artis
  • Daddy Owen
  • Eko Dydda
  • Holy Dave
  • Jimmy Gait
  • Juliani
  • Man Ingwe
                   Sarah Kierie alimaarufu Sakah K akiwakilisha Female Artist


FEMALE ARTIST OF THE YEAR
  • Emmy Kosgei
  • Gloria Muliro
  • Kambua
  • Mercylinah
  • Mercy Wairegi
  • Sarah Kiarie
                                 Kambua Mmoja wa Washitiki Wa Groove Awards 2012

GROUP OF THE YEAR
  • Adawnage
  • B.M.F
  • Kelele Takatifu
  • M.O.G
  • Maximum Melodies
  • Tetete

NEW ARTIST/NEW GROUP OF THE YEAR
  • Dan Gee
  • Everlyne Wanjiru
  • Kelele Takatifu
  • Maximum Impact
  • Willy Paul
  • Zipporah Eric

SONG OF THE YEAR
  • Exponential Potential – Juliani
  • Furifuri – DK & Jimmy Gait
  • Ghetto – Ekodydda
  • Liseme – Sarah K
  • My call – MOG
  • Ololo – Emmy Kosgei

WORSHIP SONG OF THE YEAR
  • Liseme – Sarah K
  • Nakutazamia – Mercy Wairegi
  • Niongoze – Mercylinah
  • Nisizame -Tumaini
  • Umetenda mema – Kambua
  • Waweza – Everlyn Wanjiru

ALBUM OF THE YEAR
  • Ebenezer – Mercylinah
  • Kibali – Gloria Muliro
  • Liseme – Sarah k
  • Ololo – Emmy Kosgei
  • Pulpit kwa Street – Juliani
  • Utamu wa maisha – Daddy Owen
              Mwanamuziki Wa Kiume Pekee kutoka Tanzania anayewakilisha  Tanzania katika Groove Awards.

HIPHOP SONG OF THE YEAR
  • Exponential Potential – Juliani
  • Ghetto – Eko Dydda
  • Mara hiohio – Bantu & Holy Dave
  • Mmh baba – Kriss Ehh baba
  • Ni msoo – Kelele Takatifu &Holy Dave
  • Press on – Izo & Holy Dave

AUDIO PRODUCER OF THE YEAR
  • Billy Frank
  • Gittx
  • Jacky B
  • John Nyika
  • Papa Emile
  • Saint P

VIDEO PRODUCER OF THE YEAR
  • Eagle Films
  • Eyeris
  • J Blessing
  • Prince cam
  • Sakata
  • Washamba Unlimited
Malkia wa Muziki wa Injili Tanzania Rose Muhando anayechuana Vikali na Christina Shusho katika Groove Awards 2012.

VIDEO OF THE YEAR
  • Exponential Potential – Juliani
  • Holy Ghost fire – BMF
  • My Call – MOG
  • Safari – Adawnage
  • Umetenda Mema – Kambua
  • Am Walking – Alemba & Exodus

COLLABO OF THE YEAR
  • Fresh and Clean – Kevo Juice& Jimmy man
  • Furifuri – DK &Jiimmy Gait
  • My call – MOG & Julaini
  • Ni msoo – Kelele Takaifu & Holy Dave
  • Am Walking – Alemba & Exodus
  • Welwelo – Mr Seed& Danco

RAGGA/REGGAE SONG OF THE YEAR
  • Birthday – BMF
  • Fill me – Mr T & Samukat
  • Love came me way – Verbal
  • My Call – MOG Ft. Juliani
  • Number 1 – Kevo Yout
  • Am Walking – Alemba & Exodus
Kati ya Nyimbo za Sara K zilizoingia katika Kinyang'anyiro mwaka huu ni wimbo wa "Liseme"

DANCE GROUP THE YEAR
  • Alabaster
  • Altamin
  • Detour
  • Iced
  • Saints
  • Zionists

GOSPEL RADIO SHOW OF THE YEAR
  • Gospel Sunday – Milele FM
  • Pambazuka – Citizen Radio
  • Route 104 – Hope FM
  • Shangila – Hope FM
  • Trinity Connect – Homeboyz Radio
  • Tukuza – Radio Maisha

GOSPEL TV SHOW OF THE YEAR
  • Angaza – KBC
  • Crossover 101 – NTV
  • Gospel Garage – K24
  • Kubamba – Citizen TV
  • Tukuza – Radio Maisha
  • Rauka – Citizen TV
Christina Shusho anayefanya vizuri katika Muziki Wa Injili katika Anga za Kimataifa anachuana Vikali na Rose Muhando katika Grooves Awards.

RADIO PRESENTER OF THE YEAR
  • Allan T – Homeboyz Radio
  • Amani Aila – Hope FM
  • Anthony Ndiema – Radio Maisha
  • Eudias – Radio Jambo
  • James Okumu – Hope FM
  • Mike Gitonga – Radio 316

DJ OF THE YEAR
  • DJ Krowbar
  • DJ Jonny Celeb
  • DJ Mo
  • DJ Sadic
  • DJ Sanch
  • DJ GeeGee

CENTRAL SONG OF THE YEAR
  • Nissi – Lois Kim
  • Agiginyani – Shiro wa GP
  • Marurumi – Wakabura Joseph
  • Mahindi Momu – Charles King’ori
  • Munduiriri – Carol Wanjiru
  • Muturire – Jane MuthoniHuu Ni Wimbo wa "Nakutazamia" wa Mercy Wairegi Uliongia katika Kinyang'anyiro Cha Mwaka huu

    EASTERN SONG OF THE YEAR
    • Ameru – Rosemary Njagi
    • Elote – John Mbaka
    • Jicho Pevu – Phylis Mutisya
    • Ngiti Sya Kisala – Scholla Mumo
    • Nzui Mbai – Jeremiah Mullu
    • Uu Ni Mwaka Wakwa – Peace Mullu

    NYANZA SONG OF THE YEAR
    • Batimayo – Douglas Otiso
    • Jaherana – Dr. Patrick Oyaro
    • Kendo Nisango – Geraldine Odour
    • Kinde kinde – Pastor Marvelous
    • Okumbana – Naomi Otiso
    • Ruoth Opaki – Tetete

    RIFT VALLEY SONG OF THE YEAR
    • Bong’o Longit- Gilbert Chesimet
    • Inet kei- Lilian Rotich
    • Kamura Tanet – Edina Kosgei
    • Kararan Chamet – Moses Sirgoi
    • Narue Tengek- Gilbert Segei
    • Ololo- Emmy Kosgei

    PWANI SONG OF THE YEAR
    • Ameniita – Ambrose Dume
    • Ayeiya – Kimsa
    • Ebenezer – Mercy D Lai
    • Heshima – Anastacia Mukabwa
    • Upanga – Mtawali
    • Sela Sela – Rozina Mwakideu

    WESTERN SONG OF THE YEAR
    • Bolela Yesu – Gloria muliro ft Man Ingwe
    • Buyansi – Wepukhulu
    • Omusango Kwanje – Jeff King Ft. Man Ingwe & Rufftone
    • Luhya Medley – Masinza
    • Yesu Anyala – Judith Wandera
    • Yesu ni Omuyeti – Naomi Nyongesa

    ARTIST OF THE YEAR (UGANDA)
    • Coopy Bly
    • Exodus
    • Holy Keane Amooti
    • Kingsley & Philla
    • Marc Elvis
    • S4J

    ARTIST OF THE YEAR (TANZANIA)
    • Bahati Bukuku
    • Bonny Mwaitege
    • Christina Shusho
    • Neema Mwaipopo
    • Neema Nushi
    • Rose Muhando

    ARTIST OF THE YEAR (RWANDA)
    • Aline Gahongayire
    • Beauty for Ashes
    • Dominic Nic
    • Eddy Mico
    • Lilian Kabaganza
    • Patient Bizimana
    Lilian Kabaganza from Burundi Mmoja wa walioingia katika Kinyang'anyiro

    ARTIST OF THE YEAR (BURUNDI)
    • Allelua Music
    • David Nduwimana
    • Fabrice Nzeyimana
    • Mutesi Anne Marie
    • Samuel Nvuyekure
    • Senga Dieudonne

    ARTIST OF THE YEAR (SOUTH SUDAN)
    • Daniel Lasuba
    • Jazi Rock
    • Mary Boto
    • Lam Lungwar
    • Silver X
    • Star Eagles