WAKRISTO TUMEPOTEZA SEHEMU MUHIMU SANA
AMBAYO HATUWEZI KUFIKIA VITU VYA ROHONI PASIPO HIYO IMANI:
Watanzania wenzangu, ususani wakristo kuna jambo ambalo linalo achiliwa furaha na MUNGU wetu kuja kwetu kama unaishi na IMANI na sio kuwa na IMANI maana YESU alisema ,ukiwa na IMANI kama punje ya haradani unaweza kuuambia mlima huu ng'oka nao ukatii VITUVYOTE BILA IMANI HAIWEZEKANI unapokuwa na imani unampendeza MUNGU kuna vitu ambavyo MUNGU ameahidi ambavyo tunavipokea kwa imani
ukisoma kumbu kumbu la torati 28 kunavitu vingi ambavyo utekelezaji wake ni IMANI je? unajuwa ni kwanini IBRAHIMU aliupendeza moyo wa MUNGU ? ni kwa sababu alikuwa na imani na alimwamini saana MUNGU na ndo maana alipata hata nafasi ya kuitwa rafiki wa MUNGU
LUKA mwanafunzi wa YESU, baada ya kuijua imani alidiliki kuandika yale ambayo YESU alisema mwenyewe
LK 21:15
Kwasababu mimi nitawapa kinywa na hekima ,ambayo watesi wenu wote hawata weza kushindana nayo wala kuipinga
lakini sasa huwezi kupokea siraha hii kubwa pasipo kuwa na IMANI maana hivi vyote umekwisha kupewa lakini hatuja pokea kwa kuwa hatuna IMANI
Mwenye IMANI anafundishika,hata MUNGU uingilia kati juu ya mafundisho yake,mpenda ni MUNGU anaye achilia vyote kukufuata ;afuataye baraka hana imani, aliye na imani atavumilia kila hali,akimtumai MUNGU
YESU alisema na wote watakuwa wamefundishwa na MUNGU Ili kuishikilia IMANI yao
YN 6:45
Imeandikwa katika manabii, na wote watakuwa wamefundishwa na MUNGU,basi kila aliyesikia na kujifuza kwa BABA Huja kwangu,
kwahiyo imani inajengeka kabla ya kumjua YESU na unapo okoka ndipo unazidi kukua ki IMANI,
Lakini pia leo tunaye ROHO mtakatifu ndiye anayefanya kazi ya kutupandikizia IMANI
IMANI inazaa vitu vingi sana,
mfano :hekima,maalifa,uaminifu,upendo, utu wema,kujari,na vingine vingi
YAKOBO asema ukipungukiwaq na hekima uombe dua lakini dua yenyewe ni lazima uwe na IMANI Maana maandiko yanasema kila amwendeaye MUNGU ni lazima aamini yupo kwahiyo lazima uamini
YAKO 1:5
Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa MUNGU awapae wote kwa ukalimu, wala hakemei;naye atapewa
Utapewa kama utakuwa na imani na kuamini juu ya lile uombalo,usijaribu, IMANI haijaribiwi
BWANA YESU asifiweeeeeeeeeee,,! Haleluyaaaaaaaaaa,,!
amina na MUNGU akuhifadhi na kukutetea mpendwa wangu
tuombe,,,!
BABA katika jina la YESU KRIST O
ninamuweka msomaji wa nakala hii
mikononi mwako ukamjaze imani
ya kweli na tumaini la mbinguni
ukamkumbuke pia katika uzima
wa milele na haja ya moyo wake ukampe
ni katika jina la YESU KRISTO
nimeomba na kuamini
Imeen...!
mwinjilisti Johannes R mnico
0712565676
PGM CHURCH
VINGINGITI
Askofu, BARNABAS, I ,KIMBE
0754395344 / 0653395344
KARIBU PENTEKOST GOSPEL MISSION
Huduma zote za ki ROHO zinapatikana
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni