KWA TAARIFA YAKO: NAMNA WAISLAMU, WAKRISTO NA WAYAHUDI WANAVYOTAKA KUABUDU PAMOJA
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
KWA TAARIFA YAKO unaweza kuwa unafahamu historia ya ule ukuta wa berlin ulivyowagawa Wajerumani mnamo miaka ya 60, lakini hujajua ni namna gani taifa hilo liko kwenye mchakato wa kujenga nyumba moja ya ibada kwa waislamu, wayahudi na wakristo kwa wakati mmoja, yaani msikiti, kanisa na sinagogi.
Mchungaji Hohberg, Rabbi Tovia na Imamu Kadir Sanci ©Independent |
Nyumba hiyo ya ibada itakayofahamika kama House of One, itakuwa na majengo matatu yenye maumbo tofauti, lakini yote yenye ujazo wa aina moja (idadi ya watu) ni wazo ambalo KWA TAARIFA YAKO limeanzia kutoka jumuiya ya Kikristo, tena kwa mchungaji, ambapo hadi sasa uwezeshwaji wa hali na mali ndio unaosubiriwa ili ijengwe.
Mchungaji Pfarrer Gregor Hohberg© House of One |
Mfano wa nyumba hiyo ya ibada itakavyokuwa |
Pamoja na kuwa na mitazamo tofauti kuhusu ujenzi wa nyumba hii ya ibada, wengine wakiihuisha na siku za mwisho, KWA TAARIFA YAKO pande zote zinazohusika kiimani na jengo hilo zilishafahamishwa na kuonyesha kuunga mkono jambo hilo la kipekee ambalo halijawahi kuripotiwa kwenye tasnia ya dini ulimwenguni.
Miongoni mwa viongozi wa dini hizo walioshirikishwa ni pamoja na Rabbi Tovia Ben Chorin, kiongozi wa wayahudi, ambapo alisema kwamba wanaweza kuelewana vema tu, na kwamba anatambua ya kuwa kuna ambao hawatokubaliana nalo, na KWA TAARIFA YAKO akaongeza kuwa hilo si tatizo lao, na kwamba ni kila jambo lina mwanzo wake, na huo ndo wameuanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni