MAZISHI YA MUIMBAJI NA MCHUNGAJI DEBORAH SAID KATIKA PICHA
Maelfu ya watu wakiongozwa na Katibu mkuu wa Baraza la makanisa ya kipentekoste Tanzania (PCT)Askofu David Mwasota walijitokeza kwa siku ya jana kuuga na kuupeleka kwenye nyumba ya milele mwili wa Muimbaji na Mchungaji Deborah John Said.
Ibada ya kuuga mwili huo ambayo pia ilihudhuriwa na waimbaji pamoja Maaskofu na Wachungaji mbalimbali ilifanyika katika kanisa la Maisha Ya Ushindi lililopo Ubungo External ambako ndipo alipokuwa akiongoza kanisa pamoja na mumewe Askofu John Said.
Mazishi yalifanyika katika Makaburi ya idara ya maji kata ya Makuburi, jijini Dar es salaam.
Zifuatazo ni picha tofauti zikionyesha matukio mbalimbali katika mazishi ya Muimbaji na Mchungaji Deborah John Said ambaye ni mke wa Askofu John Said
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni