Alhamisi, 17 Julai 2014


Wanamuziki Wa Injili Wawili kutoka Tanzania Christina Shusho pamoja na Gazuko Junior Wameingia katika Mashindano ya Africa Gospel Music Awards. 2014. Wanamuziki hao wameingia katika Category mbili tofauti.

Mwanamuzi Christina Shusho ambaye ameingia kwenye kinyang'anyiro hicho kwa mara ya tano mfululizo na kufanikiwa kutwaa tuzo hiyo Mwaka 2013 katika 'category' ya wanamuziki kutoka Ukanda wa Africa Mashariki na Kati mwaka huu ameingia tena katika Category hiyo hiyo. Mwaka jana Jana Mwanamuziki huyo aliingia pamoja na Wanamuziki kama Rose Muhando na Wengine kutoka Kenya, Uganda na Rwanda. Mwaka juzi Mwanamuziki Martha Mwaipaja nae aliingia katika kinyang'anyiro hicho.
Mwanamuziki Christina Shusho akiwa na Tuzo yake aliyotwaa Mwaka 2013.


Mwanamuziki wa Muziki wa Kizazi Kipya Hip Hop Gazuko Junior nae ameingia kwa mara ya kwanza katika Tuzo hizo katika Category ya Wanamuziki wanaofanya Hip hop Africa lakini pia wakiwemo wanamuziki kutoka Netherland na UK. Blog Hii iliongea na Gazuko Junior Jioni ya Leo na alieleza. "Kwa kweli Bro nimepokea kwa Mstuko Mkubwa sana habari hizi, sikutarajia na wala siku waza ila majira yangu ndio yamefika.KITU KIZURI KAMA KUFANYA KITU KIZURI NA KIKALETA MATOKEO MAZURI"

Katika Category ya Ukanda wa Africa Mashariki washindani ni:-

Katika Category hii Mwanamuziki Solomon Mkubwa anahesabiwa anatoka Tanzania wakati Tanzania wanatambua kuwa anatokea Kenya. Ikumbukwe kuwa hatakatika Groove Awards mwaka 2014 pia Solomon Mkubwa alihesabika anatokea Tanzania.

AGMA 2014 Artiste of the Yr East Africa
1. Eunice Njeri (Kenya)
2. Christina Shusho (Tanzania)
3. Jimmy Gait (Kenya)
4. Bahati (Kenya)
5. Julie Mutesasira(Uganda)
6. Jackie Senyonjo (Uganda)
7. ELIAS GEMECHU (Ethiopia)
8. Solomon Mkubwa (Tanzania)
9. Meskerem Getu (Ethiopia)
10. Sarah K.(Kenya)
11. Gloria Muliro (Kenya)
Mwanamuziki Gazuko Jr akiwa na Ze Blogger


 AGMA 2014 Hip Pop Artiste of the Yr  
 1. MOG (Netherlands)
2. SI Unit(Ghana)
3. Cjay (South Africa)
4. Pompi (Zambia)
5. VKP (Kenya)
6. Kris Eeh Baba (Kenya)
7. Gaise (Nigeria)
8. Provabs (Nigeria)
9. Andrew Bello (UK)
10. Lyrical Soldier (UK)
11. Royal Priesthood (Ghana)
12. Dolly P(UK)
13. X-Caliber (Botswana)
14. Gazuko (Tanzania)
15. Preachers(Ghana


namna ya Kupiga Kura nenda  http://www.africagospelawards.com/

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni