Jumamosi, 12 Julai 2014
MWIMBAJI MWINGINE WA MUZIKI WA INJILI NCHINI AFARIKI DUNIA
Zikiwa ni takribani wiki tatu tangu tasnia ya muziki wa injili nchini kumpoteza mmoja wa waimbaji wake marehemu mchungaji Debora Saidi, taarifa ambazo GK imezipata ni kwamba mwimbaji mwingine wa muziki wa injili Orida Njole amefariki dunia mchana wa leo katika hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Orida ambaye mpaka umauti unamfika mchana wa leo ilikuwa bado haijajulikana nini hasa kinamsumbua lakini alikuwa ameishiwa damu sana, mpaka umauti unamkuta alikuwa anatamba na album yake iitwayo 'Duniani tu wapitaji' huku kwa mujibu wa watu waliomfahamu marehemu wameeleza kwamba alikuwa mtu mchangamfu wakati wote wakati wa uhai wake na kwamba wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo chake.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe!
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni