Jumapili, 13 Julai 2014

MUNGU AINGILIA KATI KIFUNGO JELA CHA MWIMBAJI WA INJILI TANZANIA


Kifungo cha miezi mitatu jela alichohukumiwa mwimbaji wa muziki wa injili nchini Happy Kamili na mahakama ya mwanzo mkoani Mbeya, hatimaye kimebadilishwa na sasa kitakuwa kifungo cha nje cha miezi mitatu huku akitakiwa kuripoti kwa mkuu wa jela kila siku asubuhi. Happy Kamili alihukumiwa kifungo hicho na mahakama ya mwanzo mkoani Mbeya kutokana na kuendesha gari kizembe wakati anarudi nyuma na kugonga gari nyingine.

Taarifa za kubadilishwa kwa hukumu hiyo ya awali ambayo ilipokelewa kwa masikitiko na wadau wa muziki wa injili wanaotumia mitandao ya kijamii, imepatikana kupitia kwenye ukurasa wa Facebook ya mmiliki wa blogu ya Mbeya yetu bwana Joseph Mwaisango. Happy Kamili ambaye ni mke wa mchungaji Athanase Kamili wa kanisa la E.A.G.T Isanga Mbeya, amejulikana zaidi kwenye muziki wa injili nchini kupitia nyimbo zake kama 'Huwezi kubeba mzigo mwenyewe, Mpango wa Mungu lazima utimie…. alilopanga Mungu ninani apingee…

Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu blogu ameripoti hivi kupitia ukurasa wake wa Facebook

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni