Siku Ya Jumatano Jioni Kupitia Mitandao Ya Kijamii Facebook, Twitter na BBM uvumi ulienea kuwa Mwanamuziki Wa Injili Nchini Tanzania Bahati Bukuku amepoteza maisha. Watu walikuwa Wakihaha kutafuta ukweli wa habari hizo.
Kama ilivyo ada Ze Blogger alitafuta mawasiliano na Bahati Bukuku ambaye bila mafanikio namba yake haikupokelewa, ndipo jitihada zikafanyika kuongea na Rais Wa Shirikisho la Muziki wa Injili Tanzania Advocate Addo November ambaye alikanusha juu ya Ukweli wa Jambo hilo. Katika Mazungumzo na Blogger Addo alisema "Nimesikitishwa sana na kuwepo kwa uzushi huo kutoka kwa Watu, najua yamkini ni vita tu vya kiroho sababu pia dada yetu anapita sana kipindi hiki katika battle, yeye ni mzima nimeongea nae na Hatutakufa bali tutaoshi"Rais Wa Shirikisho alienda Mbali zaidi kwa kuandika katika Facebook Wall yake.
.....Ni Aibu kwa wanaoeneza Maneno ya Uongo dhidi ya Bahati Bukuku, kiukweli Bahati Bukuku ni Mzima wa Afya na nimeongea naye muda si mrefu natoaa wito tuziddi kuwaombea Wanamuziki wa Injili na kuwafunika kwa Damu ya Yesu...!! Hafi Mtu na Injili Inasonga In Jesus Name...!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni