KAATIKA UUMBAJI RUSFA ALIHUSIKA:
…natuumbe Mtu kwa mfano wetu…..” hiyo haimaanishi kwamba alikuwa akijiambia katika kikao chake Mungu mwenye nafsi tatu zilizo sawa! Kimsingi, Mungu alipokuwa akisema juu ya kumuumba Mtu, alikwisha muumba tayari katika mawazo yake, kabla ya kusema tamko lake hilo. Siku hiyo alipotamka juu ya mpango wake wa kumuumba Mtu ilikuwa ni kuweka wazi mpango wake huo na pia kuonyesha makusudi yake katika uumbaji huo.
Lakini kiukweli mkutano huo ulikuwa baina ya Mungu na Lusifa wakiwepo na malaika wote wa mbinguni, na mkutano huo ulimlenga Lusifa! Labda kabla sijaendelea niseme ni kwa nini; Kwa mjibu wa ile Mw.1:26. Hebu jiulize, kama Mungu ni nafsi tatu, na kwamba utatu huo ndiyo Mungu mmoja; je, inawezekanaje Mtu mmoja tena anayejua yote, anayeweza na Mfanya yote afanye mkutano, na kujiambia peke yake juu ya mpango Fulani aliokwisha ubuni peke yake na anatazamia kuufanya peke yake? ukiendelea ule mstari wa 27, utaona upekee wa Mungu!
Ukiendelea katika kuipeleleza Biblia utaona kuwa; Kimsingi, Mungu katika uumbaji wa huyo Mtu wa kwanza, alipenda kumshirikisha pia Lusifa kwa kuuweka wazi mpango wake huo ili kuuibua ule uovu uliokuwemo katika moyo wa Lusifa mbele ya malaika watakatfu wa mbinguni. Na kama yangetokea mapatano kati yake na Lusfa, kule kuwapo tu makubaliano japo utendaji unabakia kuwa wa Mungu, basi na Lusifa angeshiriki kumuumba Mtu! Kama hutajari ukiiangalia vema na kwa utulivu Biblia yako, bila kutanguliza ujuzi wako mwenyewe, utuona mpango mzima wa umbaji wa Mungu hadi katika lile shamba, ambalo Yule Mtu alikwenda kuishi ambako pia na huyo Lusifa alikuweko, utaona kuwa Sababu kubwa ya Mungu kuitisha kikao hicho cha “uumbaji Mtu” ulilenga kuweka wazi tofauti ambazo Mungu alikwisha ziona moyoni mwa Lusifa, naaliyekuwa akiambiwa “…natuumbe mtu kwa mfano wetu alikuwa huyohuyo Lusifa, Biblia inasema, Lusifa hakukubaliana na mpango huo na hivyo akakataa na kuwa mwasi.
Tangia hapo nafasi na kiti chake akanyang’anywa na kutupwa hapa Duniani. Naye akawa mmoja wa watawala katika hii Dunia sawa sawa na TAMAA yake! Lakini, kama ilivyo katika mabalaza na serikali za wanadamu, kiongozi anaweza kuamua kufanya jambo, na kuwashirikisha washirika wake na kuita jambo hilo wanalifanya wote! Pengine utasema ilikuwaje akasema “…Natuumbe mtu kwa mfano wetu” je, malaika nao ni mfano wa Mungu kwa vipi? Ndiyo, nao ni mfano wa Mungu! Ndiyo maana Mungu akasema “kwa mfano wetu” je, mfano wa Mungu ni upi au mfano huo ni nini aliotufanya nao ambao na Malaika pia wanao? Jibu tunalipata katika Efe.4:23-24, inasomeka hivi “Na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli” Mfano wa mungu tuliyoumbwa nao na ambao na malaika, na hata Lusfa ambaye sasa ni Ibilisi na shetani alikuwa nao ni HAKI NA UTAKATIFU WA KWELI! Kwasababu ya mda ningekuolodheshea maandiko mengi tu yanayokubali kuwa Mungu ni MMOJA tu!