WOKOVU HALISI:
KUNA AJA GANI KUIRUDIA DHAMBI ?
DHAMBI NI TESO KWAKE ALIYE FUNGULIWA ;
LAKINI KWAKE ALIYE DHAMBINI NI STAREHE;
HUONA HIVYO KWAKUWA BADO YUMO KIFUNGONI NA AMEIZOEA HALI HIYO:
Nina kukumbusha wwe ambae umemwamini YESU kuwa bwana na mwokozi wa maisha yako, kunajambo ambalo unaweza kulifanya ukaona kuwa uko sahii nakumbe haiko sahii,EFESO anema shetani analush mishale ebu simama.
PETRO anatukumbusha kuwa tumekombolewa kwa damo ya YESU na si kwa vitu vihalibikavyo kama fedha,dhahabu nk"
1 PETRO 1:18
Nanyi mfahamu kwamba mmekombolewa si kwa vitu viharibikavyo kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usio faa mlioupokea kwa baba zenu;19 bali kwa damu ya thamani,kama ya mwana-kondoo asiye na hila ,asiye na waa ,yaan,ya kristo
Kwanini kujidharau na usijione wa dhamani? dhambi inafaanya uonekane kuwa huna dhamani maana haibu hugubika udhamani wa mtu dhambi ni giza tena giza totoro ambalo huoni wala husikii jambo furani
YOHANA Anatukumbusha kuwa sisi tu wa nuru tuna liendea giza la nini?tena maana hakuna la maana huko , na wwe si wa huko maana umenunukiwa tena kwa gharama kubwa,wwe ni wa gharama bwana yasikudanganye macho.
1 YOH I:7 Bali tukeenenda nuruni,kama yeye alivyo katika nuru, twashilikiana sisi kwa sisi, na damu yake YESU,mwana wake, yatusfisha dhabi yote
Usipotembea katika utakatifu hakuna kitu na damu ya yesu haina maana kwako tena maana haupo katika njia yake tena ,wengi husema ipo neema,Usidanganyike,maana utatubu hadi lini?YESU alipo ponya watu,aliwaambia USITENDE DHAMBI TENA hakuwaambia ukitenda dhambi neema ipo njoo utubu maana alisema tena ATENDAE DHAMBI NI WA SHETANI usiwe kidumavu nilazima uonyeshe kupiga hatua,unakuwa ki roho
unapookoka tu unakuwa umeoshwa kwa damu ya YESU na kwa maji na subuni.
tena tunayo neema ya upendeleo kupewa ROHO mtakatifu.
PAULO anawaandikia wakorintho barua ya kwanza akiwaasa kuwa Adamu wa kwanza hakuwa na ROHO mtakatifu bali wao wanae basi wamsikilize ili awafundishe kuiacha dhambi.
1 KOR 15:45 Ndivyo ilivyo andikwa, Mtu wa kwanza, Adam, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuuishwa.
maana yake kimechukuliwa cha Adamu wa kale,kikaongezwa na cha MUNGU ndo wwe,kwahiyo unao ubora zaidi ya kitu cho chote.
ukijifahamu udhamani wako.hayo uliyo yaacha nyma yanini tena?dunia ya nini? itakusaidia nini? umesahauko nini? acha utoto .
PAULO alipo wakumbuka waebrania aliwaandikia barua hii:
EBR 6:1 Kwasababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya KRISTO,tukaze mwendo ili tuufikie utimilifu;tusiweke msingi tena ya kuzitubia kazi zisizo na uhai,na wa kuwa na imani kwa mungu;
Vyema tumeelewa sinaaja ya kuludia nyma ya maneno haya maana imeeleweka, cha msingi epuka mafundisho yasiofaa kwa kuwa linatajwa hapo jina la YESU
YESU hakuja ili watu wabarikiwe au wawe na utajili dhalimu NO" alikuja ili roho uliyopewa na baba imludie baba ile siku ya mwisho itakapo itajika
Leo watu wamesahau kuhubiri taba,wanahubili kubarikiwa,kufanikiwa na kuponywa lakini wanasahau YESU alipo ponya alitoa agizo kwa wale alio waponya USITENDE DHAMBI TENA nisikuchoshe mpendwa JINA LA BWANA LIBARIKIWE BWANA YESU ASIFIWE Ebu jichunguze sasa kwa kupitia somo hili ambalo ROHO wa bwana azungumza na mataifa/kanisa
MUNGU akubariki
mwinjilist Johannes R Mnico
usawawaneno@gmail.com
0712565676
PGM Church vingunguti
KARIBU
askof BARNABAS I KIMBE
Tell 0754395344 / 0653395344
PENTEKOST GOSPEL MISSION
VINGUNGUTI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni